Kanze Dena asimulia kupata ujauzito baada ya shule ya sekondari

Kanze alipanga njama ya kuficha ujauzito kutoka kwa familia yake na hata kufikiria kuasili mtoto akiwa chuoni.

Muhtasari

• Kanze Dena alifunguka kuhusu safari yake ya kwanza ya ujauzito na jinsi alivyokuwa na hofu na mama yake tangu apate ujauzito nje ya ndoa haikusikika.

• Mwandishi huyo pia alifuta dhana ya kuwa alipata ujauzito akiwa shule ya upili, na kusema kuwa ilikuwa mwaka mmoja au miwili baada ya kumaliza shule ya upili.

• Kanze alipanga njama ya kuficha ujauzito kutoka kwa familia yake na hata kufikiria  kuasili mtoto akiwa chuoni.

 

KANZE DENA
Image: HISANI

Aliyekuwa msemaji wa Ikulu Kanze Dena amefunguka kuhusu ujauzito wake wa kwanza na jinsi ulivyoathiri maisha yake.

Kanze Dena alizungumza kuhusu ujauzito wake wa kwanza baada ya shule ya upili na jinsi alivyokuwa na hofu na mama yake.

Mwandishi huyo pia alifuta dhana ya kuwa alipata ujauzito akiwa shule ya upili, na kusema kuwa ilikuwa mwaka mmoja au miwili baada ya kumaliza shule ya upili.

Kulingana na mwanahabari huyo, haikujulikana wakati wake kupata mimba  baada ya kumaliza masomo ya sekondari.

“Mara ya kwanza nilipogundua kuwa nina ujauzito wazo langu la kwanza ilikuwa nitakufa, nilikuwa na mama mkali sana, mkali sana, na hapa nilikuwa napata mimba nje ya ndoa, nilikuwa nimemaliza shule ya sekondari. Pia kuna dhana nahitaji kufichua sikuwahi kupata mimba nikiwa shuleni nilipata mimba mwaka mmoja au miwili baada ya kumaliza shule sikuolewa, na mama yangu alikuwa mkali sana siku hizo nje ya ndoa, unanyanyapaliwa kwa hivyo nilikuwa kama, nitauawa. “

Mama wa watoto wawili alipanga njia za kuficha ujauzito; kwa bahati nzuri, alienda chuo kikuu kwa masomo na kuishi katika makazi ya  shule.

 “Ilinifanya nifikirie mambo mengi sana katika mchakato huo, kwanza mama hawezi kujua kuwa nina mimba, nilikuwa naenda shuleni, nilikuwa nimejiandikisha kwenye chuo cha Secretarial and IT pale Loreto Msongari. Nilijiandikisha kuishi katika makazi ya wanafunzi chuoni ili niweze kuficha ujauzito wangu”