Peter Kioi amshauri Kanyari kuwa na mipaka mtandaoni

"Weka mipaka unaweza kufikiri watu wanakupenda kumbe wanataka kukushusha chini. ,"

Muhtasari

•TikToker Peter Kioi alimshauri Kanyari ajiheshimu kama mchungaji na awe na mipaka ambayo pia inafanya kanisa lake kuheshimiwa.

•Hii ni baada ya wanawake wengine kujitokeza kusema wanataka kuolewa na mchungaji huyo, hata alipokuwa akiwachumbia kwenye TikTok

PASTA KANYARI VICTOR
PASTA KANYARI VICTOR
Image: HISANI

TikToker Peter Kioi amemtaka mhubiri maarufu Victor Kanyari kuweka mipaka na watu anaokutana nao mtandaoni huku akimkumbusha kuwa yeye bado ni nabii ya Mungu.

Hii ilikuwa baada ya TikToker, Faith Peters, kufika katika kanisa la Kanyari na kumpa zawadi ya pakiti za kondomu, jambo ambalo liliwaacha wengi wakionyesha maoni tofauti.

Kanyari amekuwa akishirikiana na watumiaji tofauti wa TikTok na, wakati fulani, alitoa maoni ambayo yamewafanya wengi kumtaja kama mchungaji bandia.

 Kanyari alizungumza na Kioi na kumwomba aweke mipaka ambayo ingemruhusu kuheshimiwa kama mchungaji.

 “Wacha kuruhusu watu kuja kulidharau kanisa, unaweza kuniambia sasa hivi utamtolea nini Mungu, muogope Mungu, ikija kwenye suala la Chokuu naweza kusema kweli ulivuka mipaka,” alisema Kioi.

Aidha Kioi alimtaka Kanyari akome kuchezea wanawake mitandaoni na akaeleza kuwa atasikitika ikiwa Watoto wake wangeona kile anafanya mtandaoni. Pia aliongezea wengi wanataka kushusha hadhi yake kama mchungaji na wanajifanya wanampenda mtandaoni.

 "Weka mipaka unaweza kufikiri watu wanakupenda kumbe wanataka kukushusha chini." aliongeza.