Kabugi atangaza kujiingiza kujitosa kwenye siasa 2027

Kabugi ametangaza kuwania kiti cha ubunge cha eneo la Nakuru Mashariki katika uchaguzi mkuu ujao.

Muhtasari

•Kwenye mahojiano na Oga Obinna,Kabugi ameweka nia ya kujiingiza kwenye siasa 2027 kuwania nafasi ya ubunge au useneta kaunti ya Nakuru.

•Hata hivyo, hakutaja kama angekuwa mgombea binafsi au kama angejiunga na chama cha siasa.

Picha:Instagram
Picha:Instagram

 Kennedy Kabugi,mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali,alitangaza nia yake ya kujiunga na siasa za kitaifa mnamo Jumatatu, Mei 27, 2024

Kwenye mazungumzo na Oga Obinna, Kabugi alithibitisha kuwa jina lake litakuwa kwenye karatasi ya kura katika uchaguzi mkuu wa 2027.

'2027 nitashiriki kwenye kura ...' Kabugi alisema

Kabugi aliiwahakikishia watu kutoka mji aliozaliwa, eneo bunge la Nakuru Mashariki, kijana huyo mbunifu alisema kwamba atajaribu kugombea kiti cha ubunge, na ikiwa mambo hayataenda kama alivyopanga basi atajaribu nafasi ya juu zaidi kama Seneta lakini hatathubutu kuwania nafasi ya Gavana.

'Nitajaribu Ubunge ikiwa mambo hayaendi kama nilivyopanga nitagombea useneta lakini sitajaribu wadhifa wa ugavana," alisema. Hata hivyo, hakutaja kama angekuwa mgombea binafsi au kama angejiunga na chama cha siasa.

Tumekuwa tukishuhudia watu mashuhuri wengi wa Kenya  wakiwemo wanahabari, waigizaji, , wanamuziki,  na waundaji wa maudhui wakibadilisha  taaluma zao na kujiingiza kwenye siasa.Huku wengine wakifaulu na wengine kupoteza.