Mulamwah:Usinunue gari tu,nunua kitega uchumi...

Mulamwah amejivunia kuona gari lake likitumika kwa shughuli za kifahari za kiserikali baada ya kukodisha huku akiwashauri watu kutonunua gari tu bali kitega uchumi

Muhtasari

•Mulamwah ameonyesha furaha kwa kuona gari lake likitumika kwa shughuli za kifahari za serikali.

•Muunda maudhui huyo  amewataka wasanii chipukizi kujitokeza ili kushoot video za muziki kwa kuwapa gari bila malipo.

MULAMWAH
MULAMWAH
Image: FACEBOOK

Kendrick Mulamwah amefichua kuwa gari lake la  Mercedes Benz   limekuwa likifanya kazi ya kifahari haswa za kiserikali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mulamwah aliweka  video iliyoonyesha gari lake aina ya Mercedes-Benz, ambalo, kulingana naye, hukodisha wasindikizaji wa rais,waheshimiwa, na wajumbe wanaozuru wakati wa mikutano ya kilele na hafla za serikali katika Kituo cha mikutano cha kimataifa cha kenyatta (KICC).

Muunda maudhui huyo ya kidijitali alionyesha fahari yake kuona gari lake likitumika kwa majukumu rasmi ya serikali.

"Benz ya konki iko pale KICC kwa majukumu rasmi ya serikali. Najivunia kuona Benz yangu ikikodishwa na kutumika kwenye shughuli za kusindikiza rais, waheshimiwa na wajumbe wakihangaika kwenye mikutano na matukio ya serikali. Usinunue gari tu, nunua kitega uchumi, maziwa inaingia pole pole," Mulamah aliandika kwenye ukurusa wake wa Instagram.

Aidha,Mulamwah pia alitoa ofa kwa wanamuziki wajao kwa kusema kuwa yuko tayari kukopesha Benz yake bure kwa wale wanaotaka 'kushoot' video za muziki.

"Upcoming wasanii wa music videos mkuje nawapea free 💪. Inawezekana wadau," Mulamwah alisema.

Mapema Machi 21,Mulamwah aliweka wazi  mitandaoni baada ya kununua gari hilo.