Mwanamuziki wa injili Ben Githae akiri kuwa na watoto nje ya ndoa

Ninachoweza kusema tu kwamba zilikuwa baraka za Mungu na watoto wangu wote ni baraka.”

Muhtasari

•Kitu kama hicho kinapotokea, ni wazi watu wanatikisika kidogo, lakini sisi ni Wakristo, kwa hivyo tulitatua suala hilo.

•Sasa ninaweza kuwashauri vijana hawa na wanawake kutofuata njia niliyofuata.

Mwimbaji Ben Githae

Msanii wa nyimbo za injili Ben Githae amekiri wazi kuwa alichukua zamu fulani maishani zilizopelekea kupata watoto wengine  nje ya ndoa.

Githae, alizungumza katika mahojiano na Dk Ofweneke alisimuliwa swala hio ya mapenzi  nje ya ndoa.

“Nyumbani kwangu nina watoto wawili ambao wote ni wasichana. Huko nje…” alisema huku akiachia kicheko.

Alifichua kwamba licha ya kuwa mhudumu wa Neno la Mungu, alienda mbali na ndoa na kuzaa watoto nje ya ndoa.

Alisema kuwa hayo ni mambo ambayo apendi kuyazungumzia kwa sababu watoto sasa ni wakubwa vya kutosha na kuitikia kweli alichanganyikiwa.

“Sasa ninaweza kuwashauri vijana hawa na wanawake kutofuata njia niliyofuata. Ninachoweza kusema tu kwamba zilikuwa baraka za Mungu na watoto wangu wote ni baraka.”

Alipoulizwa jinsi mkewe alivyokuwa akiendelea baada ya ufunuo huo wa aibu kujulikana, Githae alinyamaza kabla ya kusema:

"Kitu kama hicho kinapotokea, ni wazi watu wanatikisika kidogo, lakini sisi ni Wakristo, kwa hivyo tulitatua suala hilo na sasa tuko sawa. Hakuna kitu maalum nilichofanya kumfanya anisamehe ni kuingilia kati kwa Bwana.

"Tatizo ni kushindwa kukubali fujo uliyoanzisha na kuishi kwa kukataa."

Aliweka rekodi hiyo kwa kusema ameoa mke mmoja pekee lakini ana wajibu kwa watoto wake wengine.

“Mimi sio mume wa wake wengi, ila tu nilifanya fujo. Nina mke mmoja tu.”

Githae alifichua kuwa hivi karibuni angerejea katika muziki, lakini kwa tahadhari.

"Nilipotoka kwenye umaarufu mkubwa hadi umaarufu sifuri, nilijificha kwa muda, kwa sababu watu wa kabila lako wanapokushambulia sio rahisi. Walakini nimekuwa nikifanya maonyesho hapa na pale. Ben Githae amerejea.”

Alithibitisha kuwa katika siku zijazo atajiepusha na nyimbo za wanasiasa.