“Haters watasema hii ni video ya AI” Waihiga Mwaura baada ya klipu akiripoti kwa Kiswahili

Alisisitiza kwamba si AI wala utaalamu wowote bali ni yeye mwenyewe aliyekuwa akiripoti kwa Kiswahili kwenye habari za Dira ya BBC Swahili

Muhtasari

• Alisisitiza kwamba si AI wala utaalamu wowote bali ni yeye mwenyewe aliyekuwa akiripoti kwa Kiswahili kwenye habari za Dira ya BBC Swahili

• “Wenye chuki bado watasema hii ni video ya AI,” Mwaura alinukuu video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwanahabari wa zamani wa runinga ya Citizen ambaye kwa sasa anafanya kazi na shirika la BBC katika kitengo cha habari za lugha ya Kiingereza cha Focus on Africa, Waihiga Mwaura amehongerwa na wengi baada ya kupakia klipu ikimuonyesha akiripoti kwa lugha ya Kiswahili.

Mwaura ni mmoja kati ya wanahabari wa BBC walioko nchini Afrika Kusini kwa sasa kushuhudia na kuripoti kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu wa kitaifa ambao uling’oa nanga mapema Alhamisi.

Akiwa nchini humo, moja ya jukumu lake lilikuwa kufuatilia kwa ukaribu shughuli nzima ya uchaguzi na kuripoti.

Kilichowafurahisha na kuwashngaza wengi kwa wakati mmoja, mwanahabari huyo mahiri katika lugha ya Kiingereza pia aliweza kuonesha uhodari wake katika lugha ya Kiswahili, kwa kuripoti kiufasaha.

Akinukuu video hiyo, Waihiga Mwaura alitania kwamba baadhi ya wasiopenda mazuri watazua dhana kwamba hiyo video imeundwa kwa utaalamu wa teknolojia ya Akili Mnemba [AI] kumuonesha akiripoti kwa Kiswahili.

Alisisitiza kwamba si AI wala utaalamu wowote bali ni yeye mwenyewe aliyekuwa akiripoti kwa Kiswahili kwenye habari za Dira ya BBC Swahili

“Wenye chuki bado watasema hii ni video ya AI,” Mwaura alinukuu video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Tazama video hiyo hapa na umpe alama kati ya moja hadi 10.