Simple Boy afuta wingu kuhusu mavazi yake :Mimi sipo Freemason

Simple boy amevunja ukimya kuhusu mavazi yake yaliyotrendi huku akitaka wakenya kumsaidia na wala si kumshurutisha mabaya anayoyafanya.

Muhtasari

•Simple Boy amekuwa akitrendi baada ya mavazi yake yaliyowatatanisha wakenya.

•Msanii huyo amesema kuwa alikuwa analeta tu kitu kigeni ndani ya tasnia ya usanii nchini Kenya.

Stevo Simple Boy
Image: instagram

Stevo Simple Boy amekanusha madai kuwa yuko freemason hii ni baada ya mavazi aliyoyavaa kuenea kote kwenye mitandao ya kijamii kwenye wimbo wake mpya wa "Shega'

Katika mahojiano maalum na waandishi wa habari wa kidijitali,Simple boy alisema mavazi yake yalipendekezwa na mtayarishaji wake wa muziki Jegedyzer.Simple Boy alisema Jegedyzer ndiye mtayarishaji wake rasmi wa muziki na yeye ndiye aliyeleta pendekezo la kuleta kitu kipya ambacho kilikuwa kimesahaulika kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya.

Kulingana na yeye hakuwa katika dini yoyote ya ibaada iwe freemason au illuminati au kujaribu ubunifu wa maudhui kwa kutumia mavazi ya waganga.

"Mimi sipo illuminati wala sipo Freemason.Siku hizi fashion zimepotea kwa muda sasa nilikuwa nahimiza watu kuwa fashion bado zipo japo zilipotea na wtu hawazitilii maanani..." Simple Boy alisema.

Aidha,msanii huyo alisema kuwa watu hawafai kumshtumu mabaya anayoyatenda ila anahitaji ushirikiano na msaada kutoka kwao na hata kumpa ushauri anapokosea.

"Wengine wanasema eti mimi si msanii ,eti mimi ni kichaa,eti siwezi ilihali naweza.Naomba watu wasichukulie mtu alivyo bali wamsaidie.Naomba wakenya wanisaidie ...."Stivo aliongeza.

Hivi majuzi,Stivo amekuwa akitrendi kwenye mitandao ya kijamii baada ya mavazi yake yaliyo na mfumo wa kinaijeria huku wakenya wengi wakiachwa na maswali mengi kichwani,kwa kudhania kuwa huenda amejiunga na chama cha Freemason.

Wimbo wake mpya wa Shega umefikisha idadi ya watazamaji laki moja na elfu thelathini na moja kule You tube chini ya siku tatu.