Mwanamuziki Prezzo,aanguka akitumbuiza wageni

Kuanguka kwake kuliibua mdahalo na maswali

Muhtasari

•Furaha ya hafla hiyo ilichukua mkondo wa ghafla wakati Prezzo alipoanguka chini, akionekana kupata kifafa

•Tukio hili liliweka kivuli juu ya kile kilichokusudiwa kuwa hafla ya kusherehekea, na kusababisha wasiwasi 

Prezzo akubali yeye ni mtoto wa mama
Rapa Prezzo Prezzo akubali yeye ni mtoto wa mama
Image: Instagram

Wakati wa makala ya The Bahati’s Empire, kipindi cha uhalisia cha televisheni kitakacho peperushwa kwenye Netflix Ijumaa, mwanamuziki maarufu wa Kenya Jackson Ngechu Makini almaarufu Prezzo alianguka akituumbuiza mashabiki.

Tukio hilo lililotokea Mei 6, lilivuta umati wa watu mashuhuri na wanahabari, huku Naibu Rais Rigathi Gachagua akihudhuria.

Furaha ya hafla hiyo ilichukuwa mkondo wa ghafla wakati Prezzo alipoanguka chini huku kiini cha kuanguka kwake kisijulikane kama inavyoonekana kwenye video zinazosambazwa mtandaoni.

Usaidizi wa haraka ulitolewa na waliohudhuria huku wakingojea usaidizi zaidi wa kimatibabu, ingawa mjadala fulani uliibuka kuhusu kufaa kwa msaada huo.

Tukio hili liliweka kivuli juu ya kile kilichokusudiwa kuwa hafla ya kusherehekea, na kusababisha wasiwasi na patashika kwa ustawi wa rapper huyo.

Wakati huo huo, uzinduzi wa The Bahati’s Empire, hatua muhimu kwa mwanamuziki Bahati na familia yake, uliendelea kama ilivyopangwa.

Bahati alielezea shukrani zake za dhati kwa mafanikio ya kipindi hicho, akihusisha na usaidizi usioyumba wa marafiki, familia, vyombo vya habari, na wafanyakazi wenzake wa tasnia, hasa kutambua jukumu la mke wake Diana Marua kama mtayarishaji mkuu.