Bahati aomba msaada wa mashabiki kufikishia Netflix ujumbe kuhusu Reality Show yao

Bahati alilalama kwamba mashabiki wakec kutoka nje ya Afrika hawangeweza kuona sura ya bintiye mdogo, Malaika kutokana na flamu hiyo kufungiwa ufikiwa na watu tu walioko barani Afrika pekee.

Muhtasari

• Hata hivyo, alishukuru Netflix kwa kumpa nafasi yeye na familia yake kuandikisha historia ya kuwa familia ya kwanza kutoka Kenya kuingia kweye kipindi cha uhalisia kwenye jukwaa lao.

Msanii Bahati ameonyesha furaha yake baada ya shoo yake ya uhalisia kuhusu familia yake kuzinduliwa rasmi kwenye jukwaa kubwa la filamu duniani la Netflix.

Usiku wa Ahamisi, Bahati na mkewe Diana waliongoza kundi la maceleb wa humu nchini akiwemo naibu rais Rigathi Gachagua katika uzinduzi wa filamu hiyo ya uhalisia ambayo ni ya kwanza kutoka humu nchini kupeperushwa kwenye jukwaa la Netflix.

Hata hivyo, baada ya kuzinduliwa rasmi, ilibainika kwamba Netflix wameifungia filamu hiyo kutazamwa tu kwa watu walioko katika bara la Afrika.

Jambo hili lilionekana kumkerekete sana Bahati ambaye alilalamika kwamba mashabiki wake wa kutoka nje ya bara la Afrika hawangeweza kuiona shoo hiyo na kuomba msaada wa mashabiki kuitaja Netlfix kwa kila komenti ili wapate kuiweka wazi kufikiwa na kila mtu kote duniani.

Bahati alisema kwamba mashabiki wake wengi kutoka nje ya bara la Afrika walikuwa wamemlalamikia kwamba hawangeweza kuona uzinduzi wa sura ya bintiye mdogo, Malaika.

“ATI WATU INJE YA AFRICA HAWAJAONA SURA YA BABY MALAIKA??? 😭😭😭 Ndio Kila Mtu Kenya na Afrika Anatazama #Thebahatisempire Lakini Bado Sehemu Yetu ya DM & Maoni Imejaa Malalamiko. Simu yangu inavuma bila kukoma kutoka kwa Mashabiki wetu wa Nje ya Bara la Afrika Wakisema kuwa hawawezi kutiririsha #BAHATISEMPIRE kwenye @Netflix Tuwafanyie Favour Wafuasi Wetu Nje ya Afrika kwa Ku-Tag @Netflix kwenye Kila Comment hapa chini tunapowaomba kuruhusu Dunia Nzima Kutazama Kipindi hiki cha Kihistoria #THEBAHATISEMPIRE,” Bahati aliandika.

Hata hivyo, alishukuru Netflix kwa kumpa nafasi yeye na familia yake kuandikisha historia ya kuwa familia ya kwanza kutoka Kenya kuingia kweye kipindi cha uhalisia kwenye jukwaa lao.

“Tunashukuru @Netflix kwa nafasi hii ya kihistoria na Ndiyo inapatikana katika kila Nchi barani Afrika- Lakini Maoni yako yamethibitisha kuwa Bahati ni Chapa ya Kimataifa yenye Mashabiki na Wafuasi kutoka Mabara yote 7 ya Dunia ... Mpendwa @Netflix Ombi Letu ni... Tafadhali waruhusu Mashabiki Wetu Duniani kote Kufurahia Show yao Pendwa #THEBAHATISEMPIRE 🙏 TAG @NETFLIX HAPA CHINI NA ENEO LAKO 👇,” Bahati alisema.