Online Media yangu ikimkera Diamond, nafukuza wafanyikazi na kufunga kampuni – Baba Levo

“Kwa hiyo wafanyikazi wangu wanatakiwa wawe makini kuhakikisha kila tunachokifanya hakitamkera Diamond Platnumz.”

Muhtasari

• Baba Levo kwamba kila kitu katika kuiendesha kinategemea mgongo wa Diaomond.

 

Image: Instagram

Mkurugenzi mtendaji wa 7media, ambayo ni kampuni ya kidijitali ya kukuza Sanaa haswa katika uchekeshaji, burudani na spoti, Baba Levo amefunguka kwamba kabla ya kuanzisha kampuni hiyo, alishafanya mazungumzo na mkubwa wake, Diamond Platnumz.

Baba Levo ambaye ni chawa wa Diamond Platnumz akizungumza na waandishi wa habari siku chache baada ya kuzindua media hiyo, alisema kwamba kila kitu katika kuiendesha kinategemea mgongo wa Diaomond.

Kulingana naye, ikitokea kampuni yake ya 7Media imemkera Diamond kwa njia yoyote ile, basi hatofikiria mara mbili bali atafukuza wafanyikazi wote na kuifunga na kurudi kuendelea kuwa chawa wa Diamond kuliko kuendelea na kitu ambacho hakimfurahishi bosi wake.

“Hili nishalitangaza na nalirudia, mimi nimefungua media nikiwa nimeshafanya mazungumzo na Diamond, ameniruhusu. Media hii ya 7media, ikimkera Diamond kwa namna yoyote, nafukuza wafanyikazi wote na kufunga kampuni, hilo linatosha,” Baba Levo alisema.

Pia alitoa tahadhari kwa wafanyikazi wake wote kuhakikisha kwamba kila wanachofanya kinamfurahisha na kumvutia Diamond maana ni kupitia furaha yake ndipo kampuni hiyo ya media itakapoendelea kuhudumu, kwani Damond akikerwa nayo kazi yao pia inakwisha.

“Kwa hiyo wafanyikazi wangu wanatakiwa wawe makini kuhakikisha kila tunachokifanya hakitamkera Diamond Platnumz.”