Vera Sidika aweka wazi cheti cha kufunga harusi ya Kiislamu na Brown Mauzo Oktoba 2020

Vera Sidika alilazimika kutoa ushahidi huo baada ya baadi ya watu kumburuza mitandaoni wakidai hakuwa ameoleka rasmi bali alimtumia kijana wa wenyewe kupata watoto na kisha baadae kumtema jalalani.

VERA SIDIKA
VERA SIDIKA
Image: INSTAGRAM

Baada ya kuburuzwa mitandaoni kwamba alimtumia Brown Mauzo ili tu kupata watoto na kisha baadae kumuacha, Vera Sidika amepinga vikali madai hayo akisema kwa kutoa vithibitisho kwamba walikuwa wameoana rasmi.

Sidika alikwenda hatua Zaidi kwa kuonesha cheti cha ndoa yao kwa mara ya kwanza mitandaoni, akifichua kwamba alifunga harusi ya Kiislamu na Brown Mauzo mnamo Oktoba 2020, na harusi yenyewe ilifanyika kinyemela bila hata watu wa familia kujua.

“Nimekuwa nikiona haya madai [kwamba Vera hakuwa ameolewa rasmi] na nadhani ni muda mimi kuweka kila kitu wazi. Kusema kweli kama nyinyi watu mlitazama Real Housewives of Nairobi, mtajua kwamba nilileta cheti changu cha ndoa kwenye muunganiko ule na kilithibitishwa,” Vera Sidika alisema.

Pia alithibitisha hilo kwa kuchapisha picha ya cheti cha harusi ya Nikkah na hata kutaja jina la Sheikh aliyesimamia shughuli hiyo akiwataka wanaobisha kumtafuta na kuthibitisha kutoka kwake.

“Nitachapisha cheti changu cha ndoa ili nyinyi wote mnikome. Halafu pia nyinyi watu mnaweza mtafuta Shekh huyo na mthibitishe kutoka kwake. Nimechoshwa na kauli za ‘hawakuwahi oana, ilikuwa ni njoo tuishi’.”

“Kwa nini nidanganye kwamba nilikuwa nimeolewa rasmi? Ama kunayo zawadi yoyote ya kuolewa inayoweza nifanya nidanganye kuwa niliolewa? Hata wazazi wangu hawakuwahi jua kama nilifunga harusi kwa sababu hatukuandaa sherehe. Tulifanya Nikkah na sheikh ambaye anajulikana sana Kenya na ilikuwa ya haraka mno,” Sidika alijitetea Zaidi.

Katika cheti hicho cha Nikkah alichokichapisha, kinaonesha kwamba harusi ilifanyika Oktoba 2020.

Sidika amekuwa akiburuzwa mitandaoni tangu mwishoni mwa juma baada ya kufichua kwamba alikuwa anaandaa tafrija ya kusherehekea kuvunjika kwa ndoa yake na Brown Mauzo  baada ya muunganiko wa miaka 3 na watoto wawili juu.

Sidika alikwenda hatua Zaidi akidai kwamba ndoa ni utapeli, jambo lililowafanya baadhi kuibua madai kwamba hakuwa ameoleka rasmi kwa Brown Mauzo bali alikuwa anamtumia tu ili kupata watoto.