Mike Sonko atoa Ksh.200,000 kwa mazishi ya Njahmby

Njahmby atazikwa Ijumaa 14,Juni 2024 kule Lang'ata

Muhtasari

•Mike Sonko ametoa Ksh.200,000 kama mchango zitakazotumika katika mazishi ya mpenzi wa reggae,Njahmby Koikai.

•Wengi wa watu mashuhuri walihudhuria sherehe ya reggae kule Quiver Lounge karibu na barabara ya Thika,iliyoekwa kama ukumbusho na kuenzi mwendazake.

Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa gavana wa Nairobi,Mike Sonko ametoa Ksh.200,000 kama mchango kwa ajili ya mazishi ya mtumbuizaji wa reggae,Njahmby anayeratibiwa kuzikwa Ijumaa 14,Juni 2024.

Kwenye sherehe zilizofanyika usiku Quiver Lounge,kwenye barabara ya Thika, wengi wa watu walihudhuria ili kusherehekea maisha ya Njambi Koikai.Ili kumuenzi na kumkumbuka.Wengi wa watu walivaa mavazi ya "kireggae".

Jahmby alijulikana sana kama mtangazaji aliyeenzi nyimbo za reggae,na alipendwa sana na mashabiki wengi wa reggae.Picha ya Jahmby ilipamba lango, ikisindikizwa na mishumaa na maua, ikiwa ni ukumbusho wa kugusa moyo kwa mtumbuizaji huyo aliyeleta furaha kwa mashabiki wa reggae kwa miaka mingi,jinsi ilivyoonekana kwenye video mtandaoni.

Baadhi ya watu  mashuhuri walihudhuria hafla hiyo; Ikiwemo ,waunda maudhui ya kidijitali kama vile Nick Kwach, Jacky Vike almaarufu Awinja, Churchill,gavana wa zamani wa Nairobi,Mike Sonko na wengine wengi.Kila mmoja alichukua muda kumkumbuka Jahmby.

Hata hivyo Mike Sonko aliguza nyoyo za wengi,alipotoa pesa taslimu Ksh.200,000 zitakazoratibika kutumika kwenye mazishi ya kigogo wa reggae,Njambi koikai.

"Hii ni laki mbili..." Mike Sonko alisema kwenye video iliyosambaa  mitandaoni.Wengi wa mashabiki wanazidi kuchangisha pesa kwa ajili ya mazishi.

Shujaa huyo atazikwa Ijumaa 14,Juni 2024 kuanzia saa nne kule Lang'ata.Ibaada maalum inatazamiwa kufanyika leo Alhamisi 13 kwenye kanisa la Nairobi Chapel,karibu na barabara ya Ngong .