Diana Marua na Bahati wafunguka kwa nini wamekuwa wakiahirisha harusi yao

Diana amesema kuwa hajajiandaa kiakili kufanya harusi lakini kuna uwezekano wa kuwa na harusi mwaka ujao.

Muhtasari

•Katika mahojiano, Bahati alifichua kuwa ni Diana ambaye amekuwa akiahirisha harusi na sio yeye

•Bahati alisema kwamba walikuwa wamepanga harusi Oktoba 20 kwa sababu ni siku ya kumbukumbu yao

DIANA MARUA and BAHATI
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji Kevin Bahati na mkewe Diana Marua wamefunguka na kufichua ni kwa nini wamekuwa wakiahirisha harusi yao.

Katika mahojiano na Spm Buzz, Bahati aliulizwa kuhusu harusi ambapo alisema kuwa walikuwa wamepanga harusi yao iwe Oktoba 20, ambayo ni siku yao ya kumbukumbu ya mahusiano.

Alisema kuwa ni Diana ambaye amekuwa akiahirisha harusi yao na sio yeye.

"Tulikuwa tumepanga harusi yetu kuwa Oktoba 20 ambayo ni siku ya kumbukumbu yetu...lakini sasa nadhani..Diana amekuwa akiahirisha sio mimi tena...anazungumzia tarehe ya mwezi wa Februari....nimekuwa nikitangaza halafu naonekana kama clout chaser...sababu unaamka unasema tarehe kumi na mbili Disemba harusi!then Diana is like eeh babe hio siku wanakuwanga busy, christmass tutakuwa tunasafiri...I'm like but it's your day it's about you...nadhani amebakia kuamua,"  Bahati alisema.

Diana alipoulizwa ni kwa nini ameahirisha harusi kwa tarehe ya mbele alisema kuwa anadhani kuwa hajajiandaa kiakili lakini anaifanyia kazi.

"Harusi hunipa msisimuko kwa tumbo...Nadhani ni kitu ambacho sijajiandaa kiakili lakini ninaifanyia kazi.. labda wakati mwingine mwaka ujao..." Diana alijibu.

Bahati pia alisema kuwa baada ya siku kumi watamfichua mtoto wao anayeitwa Malaika.

Wawili hao wamefanya harusi ya kitamaduni lakini hawajafunga ndoa kihalali.

Hivi majuzi, Bahati alimvisha mkewe Diana pete yenye thamani ya sh157,000 na kwenye chapisho lake aliandika kwamba hawezi subiri kuonyesha ni zawadi gani aliyomletea.

"157,000 Ksh ndizo nilizotumia kwa pete ya mke wangu Dubai...sasa niko kwenye mood ya kupanga harusi kubwa ya #TheBahatis na siwezi kusubiri kuonyesha zawadi nitakayo mpa...official date announcements loading," Bahati aliandika.