Stevo Simple Boy atangaza anamjengea msanii wake Machabe

Stevo alimsaini msanii wa injili, Machabe katika lebo yake ya Stevo Simple Boy Empire hivi majuzi

Muhtasari

•Jumapili Stevo alichapisha video katika akaunti yake ya Instagram akiwa katika eneo ambako anapanga nyumba hiyo inajengwa.

•Aliandika kuwa ametimiza ahadi na kumjengea msanii wake nyumba.

Stevo Simple Boy
Stevo Simple Boy
Image: Stevo Simple Boy8//Facebook

Mwanamuziki Stevo Simple Boy anamjengea nyumba msanii Machabe ambaye alimsaini hivi majuzi kwenye lebo yake.

Jumapili Stevo alichapisha video katika akaunti yake ya Instagram akiwa katika eneo ambako anapanga nyumba hiyo inajengwa.

Aliandika kuwa ametimiza ahadi na kumjengea msanii wake nyumba.

“Na hatimaye nimetimiza ahadi, nimemjengea msanii wangu Machabe nyumba, sasa wacha atie bidii kwenye mziki,” Simple Boy aliandika.

Stevo alimsaini msanii wa injili, Machabe katika lebo yake ya Stevo Simple Boy Empire hivi majuzi baada ya kujishindia fursa ya kusafiri kuenda Saudi Arabia.

Akihojiwa, Stevo alisema anataka kumjengea msanii wake nyumba. Alipoulizwa kama yeye anaweza kujikimu alisema kuwa ako sawa kwani alihamia mahali ambapo alikuwa anaishi zamani.

Hivi majuzi Stevo Simple Boy alijishindia fursa ya kusafiri kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya shoo kubwa kwa sababu ya kauli yake ya 'mefi mefi muskla'

Stevo alisema kwamba kauli yake ya ‘mefi mefi muskla’ ndiyo imemletea mafanikio hayo. Alifichua kwamba ni safari yake ya kwanza kabisa nje ya nchi katika maisha yake.

Stevo ni rapa wa Kenya ambaye hurap kuhusu masuala ya kijamii yanayoathiri jamii.

Alipata umaarufu baada ya kutoa wimbo wake “Mihadarati”