‘Kababa’ ni ya wanaume wenye pesa na Range Rover, sio kila mtu! – Dem wa FB

Alisema kauli ya ‘Kababa’ huwafaa zaidi wanaume wenye pesa na haswa wale wanaoendesha magari ya kifahari aina ya Range Rover na kuwataka warembo kutotiwa presha kuita kila mwanamume hivyo.

Muhtasari

• Katika mahojiano ya awali, Sandra Kahush alifichua kwamba kauli hiyo ni ya kuonyesha mapenzi kwa mwanamume yeyote mwenye anaonekana kujituma kimaisha, hata kama hana pesa.

DEM WA FB
DEM WA FB
Image: FACEBOOK

Mkuza maudhui chipukizi, Dem wa Facebook amekuwa mtu wa hivi punde kutoa maoni kuhusu kauli ya ‘kababa’ inayoendelea kuvutia maoni tofauti mitandaoni.

Kauli hiyo iliasisiwa na mtumizi wa mtandao wa TikTok, Sandy Kahush ambaye aliieleza kama kauli ya kuwabembeleza wanaume katika ndoa.

Wanaume wengi wamekuwa wakitoa maoni, baadhi wakihisi ndio kauli nzuri ya kuonyeshwa mapenzi na wapenzi wao wa kike huku wengine wakiipuzilia mbali kauli hiyo kuwa ni ya wanaume wanyonge.

Kwa upande wake, Dem wa Facebook anahisi kauli hiyo ni ya ya kuitwa wanaume sesheli tu na si kila mwanamume anastahili kuitwa hivyo na mpenzi wake.

Dem wa Facebook alisema kauli ya ‘Kababa’ huwafaa zaidi wanaume wenye pesa na haswa wale wanaoendesha magari ya kifahari aina ya Range Rover na kuwataka warembo kutotiwa presha kuita kila mwanamume hivyo.

“Kababa ni ya watu wenye wako na Range Rover na wako na pesa. Si kila mtu aitwe kababa. Wewe unanitumia ujumbe hapa eti kuwa kama Sandra Kahush niite kababa, wewe unaitwa tu kwa jina lako la kitambulisho,” Dem wa Facebook alisema.

Katika mahojiano ya awali, Sandra Kahush alifichua kwamba kauli hiyo ni ya kuonyesha mapenzi kwa mwanamume yeyote mwenye anaonekana kujituma kimaisha, hata kama hana pesa.

Alipoulizwa kuhusu kumsaidia mpenzi wake kulipa bili, alisema kuwa hajali kumsaidia mpenzi wake kwa kulipa bili.

Nawezafanya hivo...Najua watu husema si 50/50 lakini pia inaweza kuwa 80/20, 70/30...Sio lazima kwa mwanamume kutoa 100% kifedha kwa sababu pia wanaweza toa kihisia, kimwili na kiroho,"

"Naweza kukuweka kama uko na future...nakuweka nikiona una bidii, nikiona una future," Sandy aliongeza.