"Ndo life inaanza!" Trio Mio avunja kimya kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya KCSE

Trio Mio ni miongoni mwa watahiniwa 881,416 ambao walipokea matokeo yao.

Muhtasari

•Mwimbaji huyo aliwatia moyo waliokuwa watahiniwa wenzake na kuwahakikishia kuwa wote walijitahidi kadiri ya uwezo wao.

•Trio Mio ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote alisema, "zikam vile zinakam, sikosi usingizi mimi😂,"

Trio Mio
Image: HISANI

Mwimbaji wa muziki wa kisasa Trio Mio amewapongeza watahiniwa wote wa KCSE 2022 kufuatia kutangazwa kwa matokeo yao Ijumaa asubuhi.

Trio Mio ni miongoni mwa watahiniwa 881,416 ambao walipokea matokeo yao siku ya Ijumaa baada ya waziri wa elimu kuyaachia katika Mtihani House.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo mwenye umri wa miaka 18 aliwatia moyo waliokuwa watahiniwa wenzake na kuwahakikishia kuwa wote walijitahidi kadiri ya uwezo wao.

"Hongera kwa watahiniwa wote ambao wanapokea matokeo yao leo. Sote tulijitahidi kufikia hatua hii muhimu. Ndio maisha yanaanza na nawatakia bahati kwa yote ambayo mnapanga kufanya 💯❤️," aliandika

Trio Mio alikuwa akivuma kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii nchini huku wanamitandao wakitaka kujua alichopata.

Baadhi ya wanamitandao wadadisi walitoa makisio tofauti kuanzia A hadi D- huku wakijaribu kuwachanganya wanamitandao wenzao.

Trio Mio mwenyewe hata hivyo bado hajafichua matokeo yake halisi baada ya waziri Machogu kuyaachilia kwa watahiniwa kuangalia.

Wiki iliyopita, mwimbaji huyo mwenye kipaji kikubwa alikuwa ametoa hisia zake kuelekea kutangazwa kwa matokeo ya mtihani aliokalia.

Chini ya moja ya machapisho yake ya Instagram, shabiki mmoja alimuuliza kuhusu hisia zake kuelekea kutangazwa kwa matokeo.

"Trio results zinatoka hii wiki😂😂🔥.. Hata hivyo, upendo kwa wingi😍❤🔥," @it's nyambura.2 alimwambia.

Trio Mio ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote alisema, "zikam vile zinakam, sikosi usingizi mimi😂,"

Ina maana: (Yakuje vile yanakuja, sikosi usingizi mimi)