Mtangazaji Catherine Kasavuli avunja kimya baada ya kulazwa kutokana na saratani

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram mtangazaji huyo wa kituo cha KBC, amewashukuru mashabiki

Muhtasari
  • Gwiji huyo wa utangazaji wa habari amelazwa katika hospitali ya Kenyatta baada ya kugundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi (Cervical Cancer)
Mtangazaji Catherine Kasavuli
Image: HISANI

Mtangazaji Catherine Kasavuli amezungumza baada ya ombi la damu kutolewa ili kurejesha afya yake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram mtangazaji huyo wa kituo cha KBC, amewashukuru mashabiki kwa maombi yao na jumbe zao za kumtia moyo.

Pia kwenye ujumbe wake amesema kuwa anmatumaini ataweza kupambana na yote yanayomkabili. 

"Asanteni kwa maombi yenu na jumbe zenu za kutia moyo, tutapambana na hili," aliandika Kasavuli.

Kituo cha Runinga cha Kitaifa cha KBC Channel 1 pia kimefanya ombi la msaada wa damu kwa ajili kwa mfanyakazi huyo wake kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii.

"Mtangazaji mkongwe Catherine Kasavuli amelazwa katika Hospitali ya KNH, Mrengo wa Kibinafsi baada ya kugundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi. Kundi lolote la damu litafanya," taarifa ya KBC ilisoma.

Gwiji huyo wa utangazaji wa habari amelazwa katika hospitali ya Kenyatta baada ya kugundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi (Cervical Cancer).

Wanamitandao na mashabiki walitaia afueni ya haraka na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

jahmbykoikai: Wishing you a quick recovery and total healing in Jesus name ma'am❤️. We shall fight this and you will overcome. I love you mama❤️

djshiti_comedian: Wishing You Quick revovery ... You are a true worrior Madam Cate... Natabiri Uponyaji juu ya Maisha Yako Katika Jina La YESU.🔥🔥🔥🙌🙌🙌

_june.c_: Quick recovery Mama,stay strong❤️ so much love

paulinevulimu: Praying for you mama...much love and hugs for you❤️❤️