"Tangu mpenzi aondoke sijala!" Hamisa akiri, afichua kinachofanikisha mahusiano yake ya mbali

"Inasaidia nimpende mpenzi wangu zaidi kwani kila siku inakuwa natamani kumuona. Na kila ninapomuona i ni kama tunaanza mwanzo,” Hamisa alisema.

Muhtasari

•Hamisa Mobetto alisema kuwa mfanyibiashara huyo ambaye kwa sasa anaishi nchini China alimuaga ili kuenda kuendelea na shughuli zake za kila siku.

•Alisema kuwa maisha yake yenye shughuli nyingi na ukweli kwamba wote wawili ni waaminifu inafanya mahusiano yao ya umbali mrefu kufanya kazi.

na mpenzi wake Kevin.
Hamisa Mobetto na mpenzi wake Kevin.
Image: INSTAGRAM// HAMISA MOBETTO

Mwanamitindo maarufu wa Tanzania,  Hamisa Mobetto amethibitisha kuwa mpenzi wake kutoka Togo Kevin Sowax tayari ameondoka nchini humo.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne, Mobetto alisema kuwa mfanyibiashara huyo ambaye kwa sasa anaishi nchini China alimuaga ili kuenda kuendelea na shughuli zake za kila siku.

Mama  huyo wa watoto wawili zaidi alikiri kwamba tangu Kevin aondoke Tanzania, hajaweza kutia chochote kinywani mwake.

“Mpenzi wangu amesharudi nchini kwao. Yaani tangu asubuhi sijala. Kweli kabisa,”  Bi Hamisa Mobetto alisema.

Aliongeza, “Inabidi afanye kazi. Na mimi inabidi nifanye kazi. Tutakutana katikati.”

Mpenzi huyo wa zamani wa staa wa bongofleva Diamond Platnumz aliweka wazi kuwa yuko sawa kuwa katika mahusiano ya mbali na mfanyibiashara huyo Mtogo.

Alisema kuwa maisha yake yenye shughuli nyingi na ukweli kwamba wote wawili ni waaminifu inafanya mahusiano yao ya umbali mrefu kufanya kazi.

“Mimi naweza mahusiano ya mbali kwa sababu kwanza ni mwaminifu, pili mimi ni mtu ambaye niko bize. Nina ratiba nyingi za kazi za maisha, za watoto kwa hiyo likiwa mbali mimi pia Napata nafasi ya kufanya kazi zangu kwa ufasaha zaidi. Inasaidia pia nimpende mpenzi wangu zaidi kwa kila siku inakuwa natamani kumuona. Kila ninapomuona itakuwa namuona kama mgeni, ni kama tunaanza mwanzo,” alisema.

Kuhusu kufunga pingu za maisha na mfanyibiashara huyo, Hamisa alibainisha kuwa hatua hiyo ni mipango ya Mungu ambayo watasubiri kama itatimia. Hata hivyo, alisisitiza kuwa mpenzi huyo wake tayari ametoa mahari kwa ajili yake.

Kevin aliwasili Tanzania mapema wiki jana na Hamisa alimkaribisha na maua kabla ya wawili hao kuwa na mazungumzo na waandishi wa habari.

Katika mahojiano, Kevin alibainisha kuwa yupo nchini Tanzania kwa ajili ya mpenzi wake Hamisa. Pia alifichua angekutana na watoto wa mwanamitindo huyo, Fantasy Majizzo na Dylan Abdul Naseeb kwa mara ya kwanza.

"Itakuwa mara ya kwanza kukutana nao na siwezi kusubiri. Huwa tunazungumza kupitia simu, kupitia video ya simu. Tutakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza,” Kelvin alisema.

Kelvin alifichua kuwa yeye binafsi hana watoto lakini akadokeza kuwa anasubiri kwa hamu kupata watoto kadaa na Hamisa.

"Siwezi kusubiri," alisema.

Mtogo huyo aidha alifichua kuwa alikutana na Hamisa katika hafla ya faragha nchini China na akavutiwa naye mara moja.

Alisema ni matumaini yake kumuoa mama huyo wa watoto wawili na kuwa na familia naye katika siku za baadaye.

"Hatujui mpango wa Mungu ni nini lakini natamani twende kila mahali pamoja hadi mwisho," alisema.