Diamond akanusha madai ya kumkabidhi Mbosso gari alilokuwa amemzawidi Tanasha (Video)

Ni nadra sasa Diamond Platnumz  kuzungumzia  wapenzi wake baada ya kuachana nao lakini amefunguka kuhusu madai kwamba alimkabidhi msanii mwenzake Mbosso gari ambalo awali lilikuwa linamilikiwa na mpenzi wake wa zamani Tanasha Donna .

Simba alimua kuweka video mtandaoni akionyesha eneo lake la kuegesha magari likiwa na magari yote  pamoja na lililokuwa likimilikiwa na Donna .

Hatua yake imejiri siku chache tu baada ya Mbosso kukanusha ripoti kwamba alikuwa amekabidhiwa gari la Tanasha

Mbosso alisema, tayari bosi  wake Diamond alikuwa amemueleza kwamba kutakuwa na sakata kuhusu gari lake kufanana na la Tanasha

&feature=emb_logo

 “Hata wakati nanunua hili Gari hata Diamond mwenyewe aliniambia usipochunga mdogo wangu Gari lako litaonekana la Tanasha. Lakini nafikiria pia tunaweza kulipeleka hili gari mpaka kwa Diamod kule alafu tupige picha zikiwa zote, ile ya Mama Dangote, Tanasha na hii Hapa. Chombo changu na Nashukuru Mwenyezi Mungu ndo nimekianzia mwaka nacho, ndo linafikisha kama Mwezi hivi,”  Amesema Mbosso.

Mbosso Khan pia alitoa log book ya gari lake ili kuthibitisha kwamba halikuwa lake. Katika mahojiano hivi  maajuzi, Donna amesema halihitaji gari ambalo alipewa na Diamond kwa sababu ana lake la BMW Nairobi