Please Help! Mvulana wa Miaka amwandikia barua ya huzuni rais Kenyatta

Mvulana mwenye umri wa miaka mitano Ethan Macharia  amemwandikia barua rais Uhuru Kenyatta  baada ya yeye na mamake kukwama nchini India kwa wiki kadhaa  wlaiposhindwa kulipia gharama ya upasuaji  anoafaa kufanyiwa.

Katika barua hiyo yenye kitangulizi "Dear Mr President,"   Ethan amemraia rais Kenyatta na  wahisani wengine kumsaindia kuchangisha shilingi milioni 3.5 ili kufanikisha upasuaji anaofaa kufanyiwa . Mtoto huyo alianguka mwezi Novemba mwaka wa 2018 na kuumia kichwa walipokuwa akicheza .Baadaye hali yake ilizoroteka na kuanza kupatwa na  hali mbaya  zinazomsababishia madhara ya kimwili anapojipata bila fahamu .

Mamake Ethan ,Veronica Njeri,  amesema maisha yao yalikuwa ya kawaida hadi siku hiyo ya mkasa na wamekuwa nchini India kwa miezi 14 wakijaribu kupata pesa za kumwezesha mwanawe kupata matibabu anayohitaji kuboresha hali yake . Ethan hajaweza kurejea shuleni tangia hapo na anasema anataka kuwa mchezaji wa soka akiwa mtu mzima .