Fake friends? Papa Dennis azikwa huku wasanii wakikosa kuhudhuria mazishi

Msanii wa nyimbo za injili Papa Dennis alizikwa jana nyumbani kwa wazazi wake Matunda jimbo la Likuyani kaunti ya Kakamega, msanii Dennis aliaga dunia wiki mbili zilizopita huku akiandaliwa ibada ya wafu.

Mwili wake ulipatikana karibu na makao makuu ya chama cha  Jubilee eneo la Pangani.

Dennis alituzwa tuzo tofauti, huku wengi wa wasanii wakisema alikuwa mwenye bidii, mnyenyekevu na mwenye talanta ya uimbaji.

Lakini cha kushangaza ni kuwa wasanii wengi hawakuhudhuria mazishi hayo licha ya yao kuwa wasanii wakubwa na waliojulikana sana.

Je ni marafiki tu wa ukweli ama tu ni wa mdomo? ni jambo ambalo lilizingatiwa sana katika mazishi hayo.

Kama tunavyojua wasanii humu nchini wana umoja wa kupigiwa mfano lakini nini kiliendelea katika mazishi ya mwendazake Papa Dennis kwa sababu wengi hawakuonekana katika mazishi hayo ili kumpa mwendazake heshima za mwisho.

Wasanii waliohudhuria mazishi hayo ni kama vile, Daddy Owen,Gloria Muliro,Ringtone na Mash Mjukuu aliyekuwa  meneja wake na mmiliki wa  studio.

Daddy Owen aliandika ujumbe huu katika mtandao wake wa kijamii

"Asanteni sana watu wa Matunda. We celebrated Papa Dennis life by giving him a great send-off #RIPPapaDennis." Daddy Owen Alindika.

Mashabiki walituma jumbe zao na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

Alice Nyambu Friends are so busy holding the casket so tightly…that’s the way the could have hold his hand when he was alive.shame on…..you

Mary Dorothy How I wish Papa Dennis could wake Up just for a minute to see his after death friends and as well whip out their asses.#partyafterpartyfriends.R.I.P Dennis

Jesse Vegaz Premature death 😓💔

njeri7957 Rest in peace Papa Dennis

dun_designer Papa Dennis is smiling where he is… You guys helped him pass one of the greatest rite of passage nyinyi ni malegend big up….

Bonface Busaka Shine on your way