Raia Wa Uganda Anaswa Akisafirisha Pombe Haramu

Maafisa wa polisi kaunti ya Bungoma wamemnasa raia mmoja wa kiganda ambaye alipatikana akisafirisha pombe haramu humu inchini kutoka Kampala akielekea Nairobi,  kinyume na sheria za taifa hili.
Kamishina wa Bungoma Mohamed Maalim amesema kwamba mshukiwa alikuwa ameficha pombe hio katika gunia za avocado baada ya kudokezwa na maafisa wa usalama wa nchi ya Uganda.
Maalim amesmea kwamba raia huyo ambaye pia alikuwa inchini bila stakabadhi amefikishwa mahakamani hapo jana na kupigwa faini ya shillingi elfu ishirini na anatarajiwa kurejeshwa inchini Uganda hii leo.