Wanabodaboda Kupewa Wito Wa Kutowabeba Abiria Wasio Na Kura

Wito umetolewa kwa wahudumu wa boda boda katika eneo la Nyanza, kutowabeba abiria ambao hawajajisajili kama wapiga kura.
 
Mwenyekiti wa chama cha wahudumu wa boda boda eneo la Nyanza Nelson Odire, amewahimiza wahudumu hao kuwaagiza wateja wao kuonyesha kadi zao za kura kuanza, kabla ya kuwahudumia.
 
Kulingana na Odire hatua hii ni mojawapo ya mikakati wa kuimarisha kiwango cha wakaazi wanaosajiliwa kama wapiga kura eneo la Nyanza.
 
Aidha, amewarai wahudumu hao kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kama wapiga kura, akionya kuwa mhudumu ambaye hajasajiliwa hataruhusiwa kuegeza piki piki yake katika eneo la kubeba abiria.
 
Zoezi la usajili wa wapiga kura, uliong’oa nanga jumamatu hii litaendelea kote nchini hadi tarehe 15 mwezi ujao.