PATANISHO: Mke Wangu Ni Askari Na Naogopa Atanipiga Risasi

Bwana Stano alituma ujumbe kwa watangazaji, Gidi na Ghost huku akiomba apatanishwe na mkewe Nancy, ambaye waliachana mwaka mmoja na miezi mitatu iliyopita.

Kulingana na Stano, alitokea kazini siku moja na kupata mkewe akiwa amebeba kila kitu na kuondoka bila kusema alikoenda.

"Aliambiwa eti mimi nina mipango ya kando nje na hajawahi nipata na mtu yeyote. Mimi wakati niliamka asubuhi nikakuta tu ameenda na hadi wa leo sijajua ukweli wowote." Alieleza akifichua kuwa wamekuwa katika ndoa ya miaka minne huku akisisitiza kuwa alikuwa na mpango wa kando "Lakini mke wangu hajawahi muona."

Mwisho tuliongea aliniambia akipata nafasi ataniita tuzungumze lakini bado hatujazungumza."

"Hatujakosana na yeye shida hayuko patient, nilipelekwa Lodwar kazini. Ni bwanangu huwa tunazungumza naye kwani hadi jana tulizungumza naye. Huwa anapiga simu usiku kila mara sijui labda anadhani nina mwanaume mwingine." Alijieleza Bi. Nancy.

"Ni wasiwasi tu kuongea tunaongea naye lakini nilitaka tu anieleze kuwa tuko pamoja au la." Alijitetea Stano akiongeza kuwa aliogopa kusafiri hadi Lodwar akidhani mkewe atampangia wanaume wampige.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be