Familia ya Ababu Namwamba ya hofia maisha

Familia ya mbunge wa Budalangi anayeondoka Ababu Namwamba imeelezea hofu kuwa maisha yao iko hatarini baada ya watu wasiojulikana kuvamia makazi yao mjini Port Victoria Kaunti ya Busia.

Kulingana na mmoja wa familia hiyo profesa Tom Namwamba, kisa cha hapo jana ni cha tatu kwa muda wa wiki mbili na kusema kuwa huenda visa hivyo vina malengo ya kisiasa.

OCPD wa eneo hilo Fredrick Kagai amethibitisha visa hivyo na kusema idara ya polisi imeanzisha uchunguzi.