WEBUYE: Wanafunzi Watatu Wajeruhiwa Katika Mkasa Wa Moto Katika Shule Ya Milo

Wanafunzi watatu walijeruhiwa katika mkasa wa moto ambao uliteketeza sehemu bweni la shule ya upili ya wavulana ya Milo katika eneo bunge la Webuye Magharibi kaunti ya Bungoma adhuhuri ya Jumatano.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Albert Mutambo, wanafunzi watatu walijeruhiwa walipokuwa wanakabiliana na moto huo uliozuka saa nane mchana baada ya wanafunzi kula chakula chao cha Mchana, ikidaiwa kuwa huenda moto huo ulianzishwa na mmoja wa wanafunzi lakini ukadhibitiwa kabla ya kusababisha uharibifu.
Wanafunzi watatu waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika hospitali ya wilaya ya webuye huku Mwakilishi wadi ya Sitikho Grace Sundukwa ambaye alizuru eneo la mkasa akikashifu kisa hicho akiwataka wanafunzi kuzingatia elimu yao.

Afisa wa kukabiliana na moto katika kaunti ya Bungoma Moses Musonye ambaye alifika katika shule hiyo amewataka walimu wakuu kuzingatia sheria za kukabiliana na moto katika shule,matamshi ambayo yametiliwa mkazo na Henry Khaemba ambaye ni afisa wa kuzima Moto katika kiwanda cha sukari cha Nzoia.
-Brian Ojamaa