VIHIGA: Mwalimu Aaga Kwa Njia Tatanishi

Mwalimu wa Shule ya upili ya Ikumba iliyoko katika kaunti ndogo ya Vihiga amepatikana asubuhi ya leo akiwa amekufa katika chumba chake cha kukodisha katika mtaa wa Majengo.

Inadaiwa kuwa mwalimu huyo mwenye umri wa makamo alirejea chumbani mwake jana usiku mwendo wa saa tano na kisha kupatikana asubuhi akiwa ameaga baada ya majirani kukosa kuona dalili zake za kuamka.

Akithibitisha kisa hicho OCPD wa kaunti ndogo ya Vihiga Bw. Justine Nyaga amesema kwamba polisi wameanzisha uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo cha mwalimu huyo.