Pombe kulaumiwa kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa akili Webuye

Imebainika wazi kuwa utumiaji wa madawa ya kulevya na unywaji wa pombe kwa wingi ndio inachangia pakubwa katika ugonjwa wa akili na kusongwa na mawazo humu nchini.

Haya ni kwa mujibu wa daktari wa ugonjwa wa akili katika hospitali ya wilaya ya Webuye, Violet Kwanusu, anayesema kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali hiyo ya wanakumbwa na utumiaji wa madawa ya kulevya na unywaji wa pombe kwa wingi.

Naye chifu wa kata ya Lukusi wilaya ya Bungoma mashariki Samuel Neyombe ameitaka serikali kutenga mahali spesheli ambapo wagonjwa wa akili watahifadhiwa ili wapate matibabu na mafunzo ya kutosha.

-Brian Ojamaa