Millionea wa maisha duni aliyeuawawa alikuwa ameacha maisha ya uhalifu

Kweli hawakukosea waliposema asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu tena wakaongezea na kusema asiye sikia la mkuu huvunjika guu.

Mararfiki na jamaa za George Maina aliyeuwawa na polisi akitekeleza uhalifu katika eneo la Industrial, waliweza kumuomba awache mambo ya uhalifu na si kumuomba tu lakini walisisitiza ili awache uhalifu na kutoka katika mikononi mwa polisi.

Licha ya George kujulikana na kuishi katika maisha duni katika eneo la Mukuru kwa Jenga alikuwa millionea.

Hakuwasikia jamaa zake wala marafiki walipo muonya, marafiki wake hawakumtoroka kwa sababu alikuwa mwizi waliweza kumsaidia katika kutengeneza lori lake lililokuwa limeharibika ili wamuepushe na kesi za uhalifu na kifo cha mapema.

Lakini hakusikia chochote bali kifo cha mapema kilimkumba juma pili alipopigwa risasi na polisi kisha akafa.

Marafiki zake walisema kuwa Maina alikuwa jinai ambaye alikuwa amejulikana kwa sana na polisi pia rafiki zake.

Maina, 32, alikuwa na wenzake sita wakitekeleza uhalifu katika eneo la Industrial area walipopatwa na polisi na kupigwa risasi na polisi hao wote wakakufa.

James Mwangi ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Maina aliliambia gazetti la star jana kuwa familia ya George iliweza kumtumia polisi mmoja wa eneo la Nairobi ili aweze kuzungumza na Maina aache uhalifu lakini hayo yote alitupilia mbali.

Wakati huo polisi wa Flying Squad walikuwa wanachunguza kisa kingine ambacho Maina alikuwa amehusika kuiba katika jumba moja (go down) katika barabara ya Mombasa mwezi wa Desemba.

Polisi hawakumshika wala kumshtaki kwa maana hawakuwa na ushahidi kuwa Maina alikuwa miongoni mwa walioiba, marafiki zake waliweka wazi jambo hilo.

"Polisi huyo aliweza kuongea na Maina kwa kina na kumuonya asipo wacha kazi ya uhalifu atapigwa risasi, alipigwa risasi mwezi mmoja baadaye, tulipomuona alituambia kuwa amebadilika," Alielezea Mwangi.

Pia aliweza kusema lori ambalo polisi walilipata katika eneo la utekelezaji wizi, ndilo lililokuwa likibeba bidhaa ambazo Maina walikuwa  wanaiba katika maduka makubwa.

Na pia ndilo lori ambalo marafki zake walisaidia kulitengeneza baada ya kuwahahidi kuwa amewachana na kazi ya wizi.

Wenzake ambao hawakuwa wamejulikana waliweza kujulikana kwa majina yao, walikuwa Patrick Nzau, Wambua Maithya, Kyalo Nguli, George Muturi na Michael Mwangi.

Polisi walisema kuwa George Maina alikuwa kiongozi wao katika kundi hilo.