PATANISHO: Bwanangu alinitenga na kutorokea Thika kwa mke mwingine

patanisho
patanisho
Mwanadada, Judith, aliomba apatanishwe na mumewe bwana Patrick, ambaye walikosana na kutengana mwaka wa 2017.

"Mke wangu ako kazi Thika na kuna wakati alirudi Western huo msimu wa campaign na sikuwa nyumbani. Sasa nilikuwa Campaign na nilikuwa kwa boma la mheshimiwa fulani na sikujua mume wangu atarudi." Alisema Judith.

Aliongeza;

Kurudi nyumbani nikampata mume wangu na nikamsalimu na kwenda kulala. Alipo maliza kupiga kura hakunizungumzia na nilipomuuliza shida iko wapi hakujibu.

Nilikuwa nimesikia fununu kuwa ameoa na alidhibitisha hayo lakini sikuwa na ubaya lakini nikamuomba asitutenge na watoto kwani twaweza kuwa wake wawili kwa boma moja.

Aliongeza akisema kuwa tangia arudi Thika hajawahi muongelesha hata kama humshughulikia mara kwa mara.

Wawili hao ambao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na sita wamebarikiwa na watoto tano ambao wako Western na mama mzazi.

Patrick alikatiza mawasiliano yetu alipogundua kuwa yumo hewani kabla ya kuzima simu.

Kulingana na Judith yeye huzungumza na mama mkwe lakini hajali na maneno ya mwanao kulingana na mazungumzo yake.

"Nilitaka tupatanishwe kwani kama nilimkosea anisamehe halafu sikutaka kuwacha watoto kwa wazazi kwani itakuwa mzigo na watoto wanamaliza shule ya msingi." Alisema Judith.