Muuguzi wa Amref apatikana katika kitengo cha wagonjwa mahututi

Muuguzi wa Amref aliyeripotiwa kupotea Alhamisi amepatikana katika kitengo cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Coast General.

Familia yake ilisema kuwa Msamaria mwema aliweza kumpata Margaret akiwa hajifahamu mjini Mombasa katika kituo cha mafuta karibu Bamburi.

Kisha aliweza kuripoti kisha hicho katika kituo cha polisi cha Kadzandani, aliweza kutoka kwake saa 10:00 asubuhi Alhamisi katika mali ya Tena kaunti ya Nairobi.

Swali kuu ni je Margaret aliweza kufika aje Mombasa ilhali alikuwa anaishi kaunti ya Nairobi?

"Alitoka nyumbani Alhamisi saa nne, na hatuelewi vile alivyofika mombasa, walisema kuwa alilazwa hospitali hiyo Jumamosi, na hakuna mtu yeyote ambaye anataka kutuambia nini kilitendeka siku hizo mbili," Alisema mmoja wa jamaa zake.

Madaktari walisema kuwa Margaret Kilelu hakuwa na majeraha yoyote alipopelekwa katika hospitali hiyo. Familia yake imesema kuwa  hospitali imekataa kuwapa namba ya simu ya msamaria huyo mwema alimleta Margaret hospitalini.

"Tulipo wasili tulimpata akiwa amepoteza fahamu kisha tukampeleka katika hospitali ya Jocham kwa uchunguzi zaidi na ili kupigwa skanning,

"Alipatikana akiwa yuko sawa." Alieleza Chombo.

Familia hiyo ilisema kuwa Margaret aliweza kumpoteza mume wake Stephen Omollo kwa njia tatanishi mwaka jana Novemba kisha kliniki yake kufungwa kwa madai kuwa kuna deni hawakuwa wamelipa.

Waliongeza na kusema kuwa muuguzi huyo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Kenyatta akiugua matatizo ya akili na magonjwa mengine ambayo yanahusiana.

Kulingana na msimamizi mkuu wa CPGH Iqbal Khandwala amesema kuwa thatmini ya awali ilifichua kuwa Margaret anaweza kuwa na maambukizi ya damu, ambayo kwa sasa mgonjwa huyo anatibiwa.

"Amref walitaka kumsafirisha na ndegehadi Nairobi lakini hali yake haiko sawa, familia na marafiki wanataka kumsafirisha Margaret Kilelu kwa kutumia ambyulensi," Aliongea mmoja wao.

Mwanamke huyo alionekana kazini Amref mara ya mwisho Jumatatu, huku kutopokea simu na kisha simu yake kuzimwa kuliweza kupa familia yake wasiwasi na kisha kuanza kumtafuta.