PATANISHO: Bwanangu kazi ni kunitusi mbele ya watoto

John aliomba apatanishwe na mkewe bi Anne ambaye walikosana wiki mbili zilipita na akabeba vitu na kuondoka nyumbani.
Yeye ni mke wangu wa pili kwani wa kwanza nilimuoa na tuliwachana baada ya kumpata na mpango wa kando.

Tulikuwa tunaishi vizuri lakini wakati mtoto alianza kidato cha kwanza akaanza kubadilika. Kuna mahali nilikuwa na kazi ya duka na badala ya biashara kuendelea ilikuwa inaanguka kila wakati. Alisema John.

Aliongeza: Nilipofuatilia kumbe alikuwa anatoa fedha na kuweka kwa Mpesa yake na nilipohamisha duka nikapata ameondoka.

John alimuoa bi Anne akiwa na watoto wawili kabla yao kupata mwingine pamoja katika ndoa ya miaka minne.

"Sijarudi kwani nivile bado napumzisha akili wewe mara nyingi huwa unajifanya una madharau ndogo ndogo. Sasa pia mimi naweza toka wiki moja ili unitafute." Alisema bi Ann akimkashifu bwanake.

Atanipea mda nipumzishe akili kisha nitarudi. Huyu huskiza mambo ya majirani na akirudi nyumbani huja ananitusi mbele ya watoto sasa hiyo ni heshima gani?" Aliongeza Anne.