Massawe afunguka kuhusu ajali - Jumatano

Mtangazaji wa kipindi cha majira ya mchana - Bustani la Massawe  na kinachopeperushwa kuanzia saa nne hadi saa nane alasiri katika mawimbikasi ya Redio Jambo amechapisha ujumbe  kwa mashabiki wake katika mtandao  maridhawa wa Instagram.

Staa huyu amezamia insta story yake na kutoa ushauri wake kwa mashabiki wake kuwa wakae ange muda wowote wanaposafiri.

“Siku iliyoje! Ndo nafika chumbani baada ya kuhusika katika ajali ndogo ! Mafunzo nimeyasoma muda wowote chochote kinaweza kufanyika. Funga mkanda wa usalama kila wakati.”

Tumekusogezea hapa:

Mtangazaji Massawe alipigwa na butwaa na kuingiwa na kibuhuti baada ya tukio la jana. Wasikilizaji walimkosa Jumatano ila leo (Alhamisi) yupo yupo kuwakonga nafsi wasikilizaji wake.

Zamia uhondo hapa:

Kipindi chake huangazia sana matatizo yanakumba familia katika jamii hususan wanaume wanaopachika mabinti mimba na kuwazimia data ghafla. Massawe huwapigia simu na kuwasaidia kwa kuwaelekeza katika kituo cha kusaidia kina mama.

Jilie utamu hapa: