PATANISHO: Bwanangu alioa mke mwingine na kutorokea Mombasa

Stellah alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe akidai kuwa wawili hao wamejaliwa watoto wanne lakini mumewe amemkwepa na kuoa mke wa pili.

Kulingana na Stellah, wawili hao walikuwa wanaishi Mombasa kabla ya kukombolewa nyumba na tangia mwaka wa 2010 bwana Muhando hajakuwa akimtunza wala kujali watoto kwani hata fedha za watoto yeye hutuma mia mbili au mia tatu.

Mimi nataka tu kujua kama mimi pia ni mke wako kwani ulipooa wa pili nikama ulinitenga, nataka kujua msimamo wako mimi ni mtu mzima nitaelewa.

Bwana Muhando hata hivyo hakumpa mkewe nafasi ya kujieleza wala hakujitetea ila alisisitiza kuwa atampigia mkewe baadae watatue hayo yote.

Stellah naye alisimulia jinsi yule mke wa pili hujibu simu zake kila anapopigia mumewe, akisema kuwa kila wakati husema ni ''rong number' basi kuzuia mawasiliano kati yao.

Aliongeza kuwa anashuku wawili hao wanaishi Mombasa pamoja.

&feature=youtu.be