Hakimu mkuu wa Kiambu Brian Khaemba amejiuzulu wadhfa wake baada ya idara ya mahakama kumsimamisha kazi kwa ukiukaji wa maadili ya utendakazi .Khaemba alijipata mashakani kwa hatua yake ya kutoa agizo la kuzuia kukamatwa kwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu
Serikali yashauriwa kutafuta njia mbadala za kutafuta pesa
Serikali inafaa kuangazia njia mbadala za kutafuta pesa badala ya kuwategema walipa ushuru .mwana uchumi charles karisa amesema kampuni nyingi hazikupata faida ili kuziwezesha kulipa kodi inayotosha kuafikia malengo ya serikali
Aliyekuwa mkurugenzi wa Kenya Re ahukumiwa miaka 3 jela
Aliyekuwa mkurugenzi wa kifedha wa kampuni ya kenya Re John Kinyua amehukumiwa miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatuia ya kununua nyumba mtaani Karen kwa njia isiofaa . mtuhumiwa mwenzake Mary Ng’ang’a naye amepigw afaini ya shilingi milioni sita la sivyo ahudimie kifungo cha miezi 18 gerezani . kinyua anahudumia kifungu cha miaka mitatu jela kwa kosa tofauti .
Bei ya Petroli yapanda
Wenye magari watagharamika zaidi mwezi huu baada ya bei ya super petrol kuongezwa kwa shilingi tatu na senti saba .katyika bei mpya zilizotangazwa na tume ya ERC mafuta ya disel yamepanda kwa senti 39 ilhali mafuta taa yamepanda kwa senti 34. Lita ya petrol hapa jijini itauzw akwa shilingi 115 na senti 10.
Mandagao atofautiana na waakilishi wa kaunti
Gavana wa Uasin Gishu Jackson mandago ametofautiana na waakilishi wa kaunti baada ya kuukata mswada ambao viongozi hao wanataka kupewa shilingi bilioni 1.5 za maendeleo . waakilishi hao wanataka kila wadi kupewa takriban shilingi milioni 43 .
Mombasa kuanzisha mchezo wa gofu shuleni
Kaunti ya Mombasa inalenga kuanzisha mchezo wa gofu katika shule za umma za msingi .naibu kamishna wa kaunti Mohamed maalim amesema mchezo huo utasaidia kuwapa nidhamu wanafunzi .shule za kongowea ,likoni ,serani na maweni zimechaguliwa kwa mpango wa majaribio .
Hakimu wa Nyeri Pauline Chesang aachiliwa kwa dhamana
Hakimu wa nyeri Pauline chesang na watu wengine wanne walioshtakiwa kwa kumwua mume wake Robert chesang wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano . Jaji George Odunga amewaagiza watuhumiwa kuziwasilisha paspoti zao kortini . Sio rahisi kugundua daalili za Ebola
Sio rahisi kugundua daalili za ugonjwa wa ebola kwani hujitokeza kama magonjwa mengine .hata hivo Daktari kutoka WHO Richard Banda anasema unafaa kuwa mwangalifu kuhusu daalili kama kuharisha ,kutapika na joto mwilini endapo umezuru eneo ambako kuna mchipuko wa ugonjwa huo.
Washukiwa watatu wakamatwa Eldoret wakiwa na mifuko ya plastiki
Polisi huko eldoret wamewakamata washukiwa watatu na kunasa lori lililokuwa na mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku . mkuu wa DCI wa eldoret magharibi Linah Kabaillah amesema pia wamepata shehena nyingine ya karatasi hizo katika nyimba ya mfanyibiashara mjini eldoret .