Maafisa wa afya katika kaunti ya Kericho wapo katika hali ya tahadhari baada ya kuripotiwa kisa kimoja cha ugonjwa wa Ebola. Hii ni baada ya mgonjwa mmoja wa kike kuripotiwa kuwa na daalili za ugonjwa huo katika hospitali ya rufaa ya Kericho na baadaye kufichua kwamba alikuwa amezuru mji wa malaba ,kaunti ya Busia katika mpaka wa Kenya na Uganda kumwona mpenzi wake .
Awali mgonjwa huyo alilazwa katika hospitali ya Siloam kabla ya kuhamishwa hadi katika hospitali ya rufaa ya Kericho.Siloam imesema ilimhamisha mgonjwa huyo ili kuafikia matakwa ya arifa kutoka wizara ya afya inayowahitaji wahudumu wote wa afya kuripoti visa vya daalili za Ebola mara moja .
Ugonjwa huo umetokea DRC hadi Uganda ambako watu wawili wamethibitishwa kuaga dunia waliposafiri kwenda DRC kwa maaazishi ya jamaa yao.