Nyota wa filamu Tanzania Wema Sepetu afungwa jela

sepenga
sepenga
Nyota wa filamu na mwanamitindo  nchini Tanzania, Wema Sepetu atasalia korokoroni Segerea nchini humo kwa siku 7.

Hakimu Maira Kasonde ameamrisha staa huyu wa kike asalie kizuizini akisubiri maamuzi ya dhamana.

Soma hadithi :

Mpenzi huyu wa zamani wa Diamond Platnumz, aliingia matatani alipokosa kutii mahakama na kukosa kufika katika vikao viwili dhidi ya mashtaka ya kupatikana na dawa za kulevya.

https://www.instagram.com/p/Byz5HgSAhUg/

Hakimu alisema kuwa kesi hiyo itatajwa tena tarehe 24 Juni mwaka huu.Wema alitakiwa kufika mahakamani Mei tarehe 11 na Juni 14 ila akasusa.

Sepetu aliomba korti imsamehe kwa kukosa kuhudhuria vikao hivyo huku akitaja kuumwa na tumbo kutokana na hedhi kama kisiki kikubwa kilichomfanya asifike.

Soma hapa:

Kesi zinazomwandama Sepetu ni mbili moja ikiwemo ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya Marijuana na kuchapisha video za ngono katika mtandao wake maridhawa wa instagram.