Staa Willy Paul na majishauo sasa! Kadondosha mashine hatari

222222
222222
Fundi wa skendo na mtaalam wa muziki nchini Willy Paul sasa anajinadi na kifaa kipya cha kuendesha barabarani. Kutokana na mapato makubwa ya muziki na matamasha mbalimbali nchini, msanii huyu ameweza kuvuna hela lukuki na kudondosha chuma hatari anachokionyesha katika mitandao ya kijamii kwa mashabiki wake.

Soma hadithi nyingine:

Tazama hapa:

https://www.instagram.com/p/BzBbtMwnVwo/

Willy Paul ni msanii wa injili anayetamba na kichupa kinachokwenda kwa jina Halleluyah alichomshirikisha staa wa kike kutoka nchi jirani ya Tanzania.

Katika video hii, Pozze amejawa na furaha zaidi kuonyesha gari lake mpya huku akiilinganisha na mwanamke anayempenda. Anaongeza kusema kuwa bidii zake za kuchuma bila usingizi kumesababisha yeye kuwekeza hela ya kuinunua gari ile.

Pata hadithi nyingine hapa:

Nyota ya msanii huyu inaonekana kung'aa zaidi baada ya ubuyu kuzagaa mitandaoni kuwa anatoka kimapenzi na mwanamuziki Nandy. Minenguo ya stejini katika fiesta ya Choma Na Ngoma ilichangia mashabiki kuona Pozze amebadilika na kuasi mienendo ya kanisani.

Muimbaji huyu sasa ana ratiba kubwa ya takribani tamasha 29 zilizoratibiwa nchini na mataifa mengine ili kuwafikia na kuwakonga nafsi mashabiki wake wa muziki.

https://www.instagram.com/p/By8JoKrHfeH/