Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu
Mahakama siku ya jumatatu itasikiza kesi inayopinga zezi la kumwajiri afisa mkuu mpya wa tume ya IEBC . Pande husika katika kesi hiyo zimetakiwa kuwasilisha maombi huku korti ikishikilia kwamba agizo la kuzuia kuajiriwa kwa afisa mkuu mtendaji bado lipo . kesi hiyo iliwasilishwa mwezi uliopita na chama cha mawakili .
Dennis Itumbi ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja pesa taslimu .hata hivyo ameagizwa kuripoti katika kituo cha polisi cha muthaiga mara mbili kwa wiki kabla ya kesi hiyo kutajwa tarehe 22. Alikamatwa kuhusiana na barua iliyodai kuwepo njama ya kumwua nairobu wa rais William Ruto.
Wakati huo huo baadhi ya wabunge wamesifu uamuzi wa mahakama kumwachilia Itumbi kwa dhamana wakisema vitisho vinatumiwa ili kuwazuia wafanyikazi wa serikali kutekeleza majukumu yao .wanaitaka mahakama kumruhusu Itumbi kucheza ushahidi wa video na sauti ili kuthibitisha kwamba kuna njama ya kumwangamiza Ruto.
Wakenya zaidi wanatazama runinga na idadi ya vituo vya televisheni imeongezeka tangu uhamisho wa mtangazo hadi mfumo wa kidijitali .Ripoti mpya imesema hilo limetokana na kuwepo vya ving’amuzi vingo vya bei rahisi .
Watu wanaomiliki bunduki kinyume cha sheria hasa katika sehemu zinazokumbwa na visa vya wizi wa mifugo huko rift valley wameatakiwa kutumia msamaha uliotolewa na serikali kuzisalimisha . Mratibu wa eneo la rift valley Edward Mwamburi amesema huduma ya polisi imepigwa jeki na kuwasili kwa maafisa elfu 23 wa AP ili kufanikisha msako dhidi ya silaha haramu .
Fedha zaidi zinahitajika katika kaunti ili kutoa uhamasisho wa kuzuia utumizi wa dawa za kulevya .mwakilishi wa akina mama wa kiambu Gathoni Wamuchomba amesema kampeini za uhamisho zinafaa kufanywa katika shule za msingi kwa wanafunzi wa gredi ya pili .
Waziri wa elimu George Magoha ameagiza uchunguzi kufanywa dhidi ya madai ya matesio dhidi ya wanafunzi katika shule ya Nairobi . magoha amesema anataka kufahamu wanaotekeleza ,atesi hayo na hatua kuchukuliwa .Anataka ripoti ya uchunguzi huo kufikia wiki ijayo.
Madaktari huko Mandera wamefutilia mbali mgomo wao na kumaliza siku sita za mahangaiko ya wakaazi ambao wametatizika kupata huduma za matibabu .katibu wa tawi la muungano wao Ibrahim Maalim amesema wameafikia mkataba mpya na serikali ya kaunti hiyo.
Jopo la majaji watatu limeteuliwa na jaji mkuu David maraga kusikiza kesi iliyowasilishwa kupinga hatua ya wabunge kutaka kulipwa marupurupu ya nyumba ya shilingi elfu 250 kila mwezi .majaji Pauline Nyamweya, Weldon Korir na John Mativo ndio watakaosikiza kesi hiyo iliyowasilishwa na tume ya mishahara .
Aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Isukha central Richard Muchesia amejiua baada ya kumwua mkewe kwa kumpiga risasi katika eneo la Oangata rongai kaunti ya kajiado .Polisi wanasema wamesema wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo
Serikali imejitolea kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari kupitia hatua yake ya kuendelea kuunga mkono tafiti za wanaotumia vyombo vya habari . waziri wa ICT Joe Mucheru amesema wizara hiyo italipa pesa inazodaiwa na kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha kwamba huduma za vyombo vya habari zinamfikia kila mtu .
Mwenyekiti wa Maendeleo ya wanaume Nderitu Njoka amependekeza kwamba cheti cha ndoa kitolewe kwa wanandoa baada ya kuishi pamoja kwa mwaka mmoja ,kwa ajili ya ongezeko la la visa vya mauaji ya wanandoa . pia amewashauri wanaopendana kutafuta ushauri kwa wataalam ili kusuluhisha matatizo yao badala ya kutumia ghasia .
WANAUME ambao hudhulumiwa na wake zao hawafai kuona haya kujitokeza hadharani na kuwaripoti . mwenyekiti wa maendeleo ya wanaume nderitu Njoka amesema sheria haifai kuwapendelea wanawake wanaowadhulumu waume zao kwani wanaume pia ni waathiriwa wa dhulma za kinyumbani .
Wasimamizi wa shule wanafaa kuzisikiliza lalama za wanafunzi ili kuepuka visa vya rabsha shuleni .mtalaam wa masuala ya elimu Eugen Ojiambo amesema wakati mwingi wasimamizi wa shule huwa hawawahusishi wadau wote kushughulikia masuala yalioibuliwa na wanafunzi .
Idadi ya magezeti ya kila siku yanayouzwa nchini imekua ikupungua .Ripoti kuhusu vyombo vya habari imeonyesha kwamba kumekuwa na upungufu wa asilimia 33 wa kiasi cha magazeti yanayouzwa nchini tangu mwaka wa 2013 . ingawaje redio husikizw ana watu wengi ,watu hungoja kusoma magazeti ili kuthibitisha waliosikiza au kutazama katika runinga .