Mchungaji akamatwa kwa kumkashifu rais Museveni

Joseph.Kabuleta.000
Joseph.Kabuleta.000

Mchungaji Joseph Kabuleta ni raia wa hivi punde wa Uganda kujipata mashakani kwa tuhuma za kumkashifu au kumkasirisha rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.

Bw Kabuleta, alikamatwa na maajenti wa usalama ambao hawakuwa na sare rasmi mwendo wa saa kumi na moja jioni, Ijumaa iliyopita mjini Kampala.

Maafisaa hao aidha hawakuwa na gari rasmi la kazi na wakati wa kumkamata mchungaji huyo hawakuoa sabababu yoyote ya kuchukua hatua hiyo.

Kabla ya kukamatwa kwake Bw. Kabuleta alikua akiendesha kampeini kali katika mitandao ya kijamii ambapo alikua akiikosoa Utawala uliyo madarakani na familia ya Rais.

Katika waraka wa hivi karibuni kwa jina "Mafia Empire and the Transition",ambao ulichapishwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook mnamo Julai 8, Bw. Kabuleta alielekeza lalama zake hususan kwa mwana wa kiume wa Rais Museveni na mshauri wa ngazi ya juu wa oparesheni maalum, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba. Alisema mpango mzuri ni kuhakikisha Jenerali Muhoozi hamrithi baba yake kama rais.

"Tayari Jenerali Muhoozi amekuwa akitumwa kumwakilisha baba yake kwa mikutano ya kimataifa na pia kukutana na mabalozi na viongoziwengine wa ngazi za juu na kuelezea katika mtandao wake wa kuhusu ziara hizo ," ilisema sehemu ya ujumbe wa Bw. Kabuleta.

Aliongeza kuwa: "Huenda Baba yake ana mpango wa kustaafu kimpango baada ya kuchakachua uchaguzi wa mwaka 2021 na kuchukua jukumu la kumshauri mwanawe huku akiendelea kundesha biashara ya kampuni ya familia inayofahamika kama Uganda.

"Au pengine mageuzi yakifanyika ndani ya chama cha NRM na taifa lianze mfumo wa utawala wa kibunge ambapo chama kilicho na wabunge wengi kunachukua uraisi."

N akumaliaza: "Mpango wowote walionayo, Lakini nahisi mambo huenda yakabadilika. Himaya ya Mafia imeanza kuporomoko na Uganda itarejea mikononi mwa Waganda."

-BBC