PATANISHO: Kondoo ndio ilitutenganisha na mke wangu

Alex mlima Elgon na mkewe bi Lilian ambaye walikosana na akaondoka miezi mitano iliyopita.

"Nimeishi na mke wangu miaka miwili na kuna kondoo niliuza bila kumwelezea na baada yake kurudi kwenda kuangalia hakupata kondoo. Alipouliza nikamwambia nimepeana na nika ahidi kununua mwingine." Alieleza.

Isitoshe mama mkwe alianza kumgombanisha na hapo Lilian akaondoka.

Alex anasema amejaribu kumfuatilia mkewe lakini bado hajapata hakikisho kuwa atarudi kwa ndoa yao.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na wamejaliwa mtoto mmoja ambaye aliondoka na mkewe.

Juhudi zetu za kumtafuta bi Lilian hazikufua dafu kwa mara ya kwanza na pindi tulipompata hakuwa tayari kuzungumza nasi wala bwanake na alisitisha mawasiliano yetu aliposkia sauti ya Alex.

Ujumbe wake Alex kwa Lilian ulikuwa,

Namwelezea akae vyema na akumbuke arudi kwake. Namuomba msamaha na nampenda sana.