Ahadi ni Deni:Rais Magufuli aleta Tausi wanne aliomwahidi rais Kenyatta maajuzi (Picha)

Rais wa Tanznia John magufuli  ametimiza ahadi yake ya kumpa mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta tausi wanne  . Rais Kenyatta aklikabidhiwa zawadi hiyo siku ya ijumaa na balozi wa Tanzania humu nchini  Pindi Hzara Chana . Akizungumza baada ya kupokea ndege hao  rais Kenyatta alimshukuru Magufuli  akisema ndege hao   wanaashiria umhimu wa upendo ,umoja na undugu kati ya Kenya  na Tanzania .

Magufuli  alikuwa amemwahidi rais Kenyatta kwamba nangempa tausi hao kama zawadai wakati Kenyatta alipomtembelea kwa ziara ya kibinafsi ya siku mbili  mwezi uliopita . Alifanya utani kwamba pindi tu rais Kenyatta alipokanyaga   katika boma lake ,alianza kuwatamani tausi hao  ambao pia walionekana kumfurahia .Magufuli,  hata hivyo alisema kwaba iwapo ndege hao watazaana ,basi  Uhuru anafaa kuwarejesha wanne Tanzania .