He's NOT a dead beat! Bahati atetewa na baby mama

Yvette Obura aliyezaa mtoto na mwanamuziki wa gospel  Bahati  ameanza kumtetea msanii huyo baada ya wawili hao kuwa katika pande zinazokinzana kwa muda mrefu .  Obura amepuuza madai kwamba Bahati huwa hatoi hela za kumtunza  bintoye .

katika hafla ya kujibu maswali katika instragram  Yvette amebainisha wazi kwamba hana  tatizo kuhusu  juhudi za Bahati kumtunza mwanawe . Shabiki mmoja alikuwa ameashiriia kwamba mwimbaji huyo hakuwa akitekeleza majukumu yake kama baba .

Mambo hayajakuwa  rahisi kati ya Bahati na Yvette  baada ya msanii huyo kushtumiwa kwa  kutelekeza majukumu yake kama baba  na kilichofuata ni majibizano kati yao lakini baadaye waliafikiana na kukubali kufanya uzazi wa pamoja kwa binti  yao .

Yvette  kwa wakati mmoja alifunguka na kufichua jinsi alivyolazimika kulala njaa kwa siku kadhaa alipojifungua bila kupata usaidizi kutoka kwa Bahati  lakini sasa bifu hiyo imezikwa na wanaheshimiana .