Maana ya jina hilo iliwasilishwa kortini mwaka wa 2018 na mtu moja wa kushiriki michezo ya kubashiri Lesaloi Selelo, ambaye alidai kwamba kutoza kodi kwa kiasi cha fedha alizoshinda mtu anayeshiriki mchezo huo ni ukiukaji wa katiba .Pevans E. A. Limited, Bluejay Limited na Acumen Communication Limited ambao walihusishwa katika kesi hiyo walidai kwamba pesa anazoshinda mtu katika michezo hiyo sio mapato na hazifai kutozwa kodi .Betway baadaye iliwasilisha kesi kama hiyo mwaka wa 2018 ili kupata tafisiri ya ‘pesa anazoshinda mtu ‘ lakini kesi hizo zikajumuishwa kuwa moja kwa sababu zilikuwa zikishughulikia masuala yanayofanana .
Mahakama ilifutilia mbali kesi hiyo siku ya alhamisi hatua inayomaanisha kwamba tafisiri ya KRA kuhusu pesa alizoshinda mtu katika michezo ya kubashiri zitatozwa kodi .KRA ilizidhiinisha kampuni 10 mbazo hazikupewa upya leseni Julai tarehe moja kwa sababu ya maswali kuhusu utekelezwaji wa kanuni za ulipaji kodi.Betway, OdiBets, Mozzartbet, Ken Bookmakers, Lucky 2u, Eazi Bet, Kick off, Eastleighbet, Palms Bet na Bet zilipokea idhini ya kuhudumu Julai tarehe 22 lakini Betin na SportPesa, ambazo ni miongoni mwa kampuni kubwa za michezo ya kubashiri hazikuwa katika orodha ya KRA ya kampuni zenye idhini ya kuhudumu .