Susumila ajibu madai kuwa majini hayaandiki nyimbo

Susumila amerejea na kuwajibu wanaomkashifu kwa madai kuwa yeye anatumia ushirikina ili kufadhilisha muziki wake pamoja na biashara zake.Susumila ambaye kwa sasa anataba na kibao, "Warembo" amekanusha madai yote yanayo muhusisha na utumizi wa Majini kwa kusema kuwa majini hayawezi andika nyimbo.

"Nimelisikia hilo kwa muda mrefu sasa ila ningependa watu wajue kuwa majini ama nguvu za ushirikina huwa haziandiki mishororo ya mashairi au nyimbo."

"Wimbo wangu mpya una hisia tamu hasa ukisikiliza mishororo yenyewe kwa udani. Madai hayo yote najua yanatolewa na maadui wangu wanaopania kunikwaza kila wakati na katika kila jambo nifanyalo maishani mwangu."

Susumila hata hivyo aliwahimiza wanaoeneza uvumi kumuhusu waendelee tu kwani yeye hatowajali na atazidi kuimarisha maisha yake." Najua pia watasema kuwa nimeedelea kimaisha kwa sababu gavana wa Mombasa, Hassan Joho alinisaidia ila mimi nasema kuwa ni sawa tu kwani lazima mambo kama haya yatokee."