Patanisho: Nilipata P2 kwa nyumba yake nalipomuliza akakasirika

Bwana Kelvin,34, alipiga simu akiomba apatanishwe na bibiye Bi. Josline,29,  ambaye walikosana siku ya Jumapili baada ya kumtembelea na kupata dawa za kujikinga na mimba. Kelvin anashuku kuwa mkewe ana uhusiano na mwanamume mwingine wanaofanya kazi mahali moja.

 "Aliniambia kuwa alikuwa anaenda mjini Nakuru  kwa ajili ya kazi na aliporejea hakuniambia. Nilimpigia simu nikitaka anieleze kama amerudi lakini aliniambia hajarudi ila nilikuwa najua amerejea hapa mjini Nairobi. Niliamua kwenda kwake na nilipofika nilipata tembe za P2 ambazo hutumiwa kujizuia kupata mimba.Nilipomuuliza alikataa na niliporudi nyumbani tulitumiana jumbe mbaya mbaya sana."

Ndoa ya wawili hawa ilianza mwaka 2009 na imedumu kwa muda huo wote licha ya kwamba hawajawahi kufunga ndoa huku wakiwa wazazi wa mtoto mmoja pekee.

 Bi. Josline kwa upande mwingine anasema kuwa Bwana Kelvin amemkosea sana hasa kwa maneno yake makali.

"Hio siku ilikuwa tukutane ila yeye alijileta kwangu na akapata hizo P2 juu mimi nilishamove on. Alinikasirisha sana hasa baada ya kupiga simu kazini kwangu na sasa kazi yangu imo mashakani.Huyu jamaa alinitusi sana hata akatusi mama yangu. Tangu Mwaka 2009 hataki tuoane na mimi nisha move on."

"Alinifukuza kwake nikiwa na mtoto wa miezi mitatu na sasa akona watoto watatu wengine ukiachana na huyu mtoto wetu."

Bwana kelvin alijaribu kumuomba mkewe amsamehe ila Bi. Josline alikwamilia kwa uamuzi wake na kusema kuwa yeye amepata mwanamume mwingine na hivyo Kelvin anapaswa kumsahau na aendelee na maisha yake kwa sasa.

Hata hivyo kama ilivyo ada ya Patanisho, Vituko ni jambo la kawaida na hii leo bwana Kevo alivunja mbavu baada ya kusema kuwa wanawake ni kama Kuku,wanakula huku kisha wanapanguza mdomo na kukula kwingine kama vile bibiye alivyo mfanyia.

Baada ya kusikiliza kwa umakini, Gidi na Ghost walimshauri kevo akubali kuachwa na aendelee na maisha yake.