Ukocha wa Harambee Stars ulijaa songombingo tele. Ghost Ataja masaibu

Ghost_Ushuru__1568815112_31029
Ghost_Ushuru__1568815112_31029
Mtangazaji wa kituo cha Jambo Ghost amesimulia masaibu yaliyopelekea yeye kujiuzulu ukocha wa timu ya kitaifa.

Katika mahojiano, Ghost amesema kuwa kuchelewesha kwa mishahara kulichangia sana.

Soma hadithi nyingine:

"Maswala ya kulipwa yalikuwa ni tatizo kubwa. Nawadai milioni kadhaa. Nimekuwa na rais wa shirikisho akanieleza kuwa wanakifa wataleta hela yangu kwa matanga haraka sana..."

Ghost amesema kuwa kipindi na alipokuwa akihudumu kama kocha wa Harambee Stars kilikuwa kigumu sana.

Amemsifia mkewe kwa kuwa katika mstari wa mbele wa kuisetiri familia wakati huo.

"Nilianza ukocha wa timu ya kitaifa mwaka wa 2002 hadi mwaka wa 2005 nikajiuzulu kwa mara ya kwanza."

Soma hadithi nyingine:

Ghost Mulee anataja sababu za kujiuzulu mara kwa mara.

"Kisa na maana ni ushenzi wetu wa kutolipa watu pesa. Kuna wakati mmoja nimefanya kazi kwa miezi 8 bila kulipwa."

Ghost sasa anamiliki Liberty Sports Academy ambayo anaitumia kama sehemu nzuri ya kukuza vipaji.

Soma hadithi nyingine:

"Bado nipo kwenye kabumbu. Nina academy ya Liberty Sports Academy  ambapo Michael Olunga ametokea. Ni vijana wengi ambao tumewakuza. Nikitoka kufanya utangazaji huwa naingia katika academy yangu."