Ghost atoa sababu za kuchoshwa na binadamu. Ataja starehe zake (+ Video)

69516079_169524644097474_5463231092729727764_n_1___1568884130_66081
69516079_169524644097474_5463231092729727764_n_1___1568884130_66081
Mtangazaji wa kipindi kinachoongoza nchini cha asubuhi Patanisho amefunguka kuhusu maisha yake.

Ghost katika mahojiano ametangaza kuwa wanadamu wamemchosha na kwa hivyo ameweza kuzamia katika maswala ya kujipa raha.

"Binadamu wamenichosha. Wengi ni waongo. Wengi hawasemi ukweli..."

Soma hadithi nyingine;

"Kwa ivyo mimi nikienda nione wanyama nafurahi zaidi..."

"Nikiona simba anaua nafeel poa sana. Ataua mara moja ale amalize lakini binadamu mara ataka hiki ataka kile. Tuna tamaa nyingi."

"Kwa hivyo nikikaa na wanyama nafeel poa. "

"Nikisikiliza muziki unanituliza roho..."

Soma hadithi nyingine;

Ghost amesema kuwa yeye hana mambo mengi. Ni mstaarabu sana,

"Ghost Mulee ni jamaa mmoja very simple. Jamaa ambaye anapenda raha kwanza. Napenda yaani kufurahia."

Staa huyu wa utangazaji anaelewa kuwa maisha ni mafupi sana,

"Unajua wanasema kuwa maisha ni mafupi. Sipendi kukasirika, kwa sababu najua siku yangu ya kukasirika ni nikifa."

Soma hadithi nyingine;

"Kaburini pale hakuna kutabasamu na mtu. Nikichukia nachukia dakika moja ila sikai na hasira. Maanake hasira ukikaa nayo unazidi kuzeeka."