Wabunge watishia kuwatimua kazi Mawaziri Munya, Kiunjuri

Wabunge  hususan kutoka maeneo yanayokuza chai na kahawa wamemrai Rais Uhuru Kenyatta kuwapiga kalamu mawaziri wake wanaozembea kazini.

Zaidi ya wabunge 20 wanahoji kwamba mawaziri Peter Munya wa Biashara na Mwangi Kiunjuri wa Kilimo wang'atuke mamlakani.

Mawaziri hao wanatuhumiwa kwa utendakazi duni katika wizara zao.

Akihutubia mkutano wa waandishi wa habari katika majengo ya Bunge Jumatano, Wabunge wakiongozwa na mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria walisema watafanya kila wawezalo kuhakisha kwamba masaibu ya wakulima yanaangaziwa.

Kwa kipindi kirefu sasa wakulima wa kahawa na chai wamekuwa wakilalamikia pato duni kutokana na kushuka kwa bei za bidhaa hizo muhimu katika soko.

Viongozi hao hasa kutoka maeneo ya Mlima Kenya na Bonde la Ufa pia walimkosoa waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri kwa kuruhusu madalali ambao wanaofahamika na  KTDA kuwalaghai  wakulima.

Aliongeza kusema kwamba watatumia kila njia kuwatetea wakulima ikiwemo kuwalisha mswada bungeni wa kutokuwa na imani na baadhi ya mawaziri.

"“Where you see smoke there is fire," Kuria alisema alipoulizwa ikiwa anadhamiria kupeleka mswada bungeni ya kuwango'a mamlakani mawaziri wazembe.

"Tunataka bei nzuri kwa chai yetu, tunataka serikali ianze kuchukilia suala la kilimo kwa umakini," Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro alisema.

Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua alisema 'Uhuru alikuwa na nia nzuri kwa wakulima wa chai na kahawa lakini nia yake nzuri inaharibiwa kimaksuudi na mawaziri wa baraza waliopewa jukumu la kuboresha sekta hiyo inayodhorora.'

"Tangu Munya alipopewa idara ya Biashara, hajawahi zuru katika kiwanda kiwanda chochote cha chai na kuwashirikisha wakulima katika uundajisera. Kile anajofanya ni kuunda jopo kazi ambayo haina ufaahamu nzuri kuuhusu maskahi ya wakulima." alisema.