Nyota Eliud Kipchoge kutimua Viena kesho, Ineos ina maana gani?

kipchoge
kipchoge
Jina la Ineos limeteka anga huku mahiri na bingwa wa Olimpiki katika mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge akisubiriwa kutwaa ushindi hapo kesho.

Nyota huyu aliondoka kwenda Vienna ndani ya jeti la kifahari aina ya Gulfstream G280.

Eliud alisema kuwa ana matumaini sana ya kuvunja rekodi hiyo anayotarajiwa kukimbia mbio hizo kwa chini ya saa mbili wikendi.

Soma hadithi nyingine:

Ineos ni kampuni nambari moja duniani na ya kibinafsi inayohusika na utengenezaji wa kemikali na mafuta iliyopo nchini Uingereza na ina makao makuu mjini London.

Kampuni hii ina ofisi zilizosajiliwa Lyndhurst, Hampshire, na Uingereza.

Jim Ratclifee ndiye muasisi na mwenyekiti.

Jina la Ineos lina maana ya (Inspec Ethylene Oxide Specialties)

Baada ya kuwasili Uingereza, Eliud Kipchoge alianza siku yake ya kwanza huko Vienna kwa kufanya mazoezi ya mbio hizo pamoja na wanariadha wenzake wa pembeni.

Soma hadithi nyingine:

Kipchoge ambaye alifika Vienna Jumanne  alionekana mchangamfu huku akianza maandalizi hayo kwa kufanyia mwili wake mazoezi maalum ana kunyosha viungo.

“Nina hamu sana ya kushiriki mbio hizi na ni matumaini yangu kuwaona wote wikendi hii.” Kipchoge alisema.